" JESHI LA POLISI LAENDELEA KUMTAFUTA HUMPHREY POLEPOLE KUHUSU TUHUMA ALIZOZITOA

JESHI LA POLISI LAENDELEA KUMTAFUTA HUMPHREY POLEPOLE KUHUSU TUHUMA ALIZOZITOA

 Jeshi la Polisi Tanzania, lingependa kutoa taarifa kuwa lilifungua jalada la uchunguzi na linaendelea kuchunguza tuhuma mbalimbali ambazo amekuwa akitoa Humphrey Herson Polepole toka Julai 2025.

Tuhuma ambazo ametoa na anaendelea kuzitoa kulingana na jinsi alivyozielezea zinaashiria uwepo wa makosa ya kijinai na kwa mujibu wa sheria zinahitaji ushahidi wa kuzithibitisha zitakapo wasilishwa mahakamani.

Tuhuma hizo amekuwa akizitoa kupitia mitandao ya Kijamii.

Baada ya kufungua jalada na kuanza uchunguzi, Jeshi la Polisi mbali na kukusanya ushahidi, limekuwa likifanya jitihada za kumpata ili aweze kutoa maelezo/ushahidi na vielelezo vitakavyo thibitisha tuhuma hizo ili kuwezesha hatua zingine za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na ndivyo utaratibu wa kisheria ulivyo.

Hivyo Jeshi la Polisi kupitia taarifa hii linaendelea kumwelekeza afike katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ili aweze kutoa maelezo/ushahidi kuhusiana na tuhuma ambazo amekuwa akizitoa kwa umma kupitia Mitandao ya Kijamii.


Imetolewa na:

Msemaji wa Jeshi la Polisi

Makao Makuu ya Polisi

Dodoma, Tanzania.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post