Askofu Ayubu Mwakibinga akiongoza waumini wa Deliver
Hope Church of All Nations katika maombi maalumu ya mfungo wa siku 38 kuliombea
amani ya Taifa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, uliofanyika katika makao
makuu ya kanisa hilo yaliyopo Kijiji cha Nyanende, Kata ya Kizumbi, Manispaa ya
Shinyanga.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, Kanisa
la Deliver Hope Church of All Nations limetamatisha rasmi mfungo na maombi ya
siku 38 yaliyoanza tarehe 1 Agosti 2025 kwa lengo la kuliombea Taifa la
Tanzania kuelekea uchaguzi huo.
Akizungumza mgeni rasmi, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya
ya Shinyanga, Richard Makoye, amepongeza Deliver Hope Church of All Nations
kwa kujitolea kuandaa mfungo huo muhimu kwa Taifa huku akisema kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wa
taasisi za dini katika kudumisha amani, mshikamano na utulivu, hasa katika
kipindi hiki ambacho Taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu.
"Maombi yenu yana mchango mkubwa
katika kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani na utulivu. Serikali inatambua
mchango wa makanisa na taasisi zote za dini katika kudumisha mshikamano wa
kitaifa. Nitoe wito kwa viongozi wa dini na wananchi wote kuendelea kuombea
nchi yetu, ili tupate viongozi wenye maono ya kweli, moyo wa kulitumikia Taifa
na kuwaletea maendeleo wananchi," amesema Makoye.
Aidha, amesisitiza kuwa Serikali itahakikisha
inasimamia uchaguzi kwa uadilifu, uwazi na haki, huku akihimiza wananchi wote
kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya uchaguzi.
Maombi hayo yalifanyika katika makao makuu ya kanisa
hilo yaliyopo Kijiji cha Nyanende, Kata ya Kizumbi, Manispaa ya Shinyanga,
chini ya uongozi wa Askofu na Mwasisi wa Kanisa hilo, Ayubu Mwakibinga, ambaye
amesisitiza kuwa maombi hayo yamelenga hasa kuombea amani ya Taifa, mshikamano
wa kitaifa na upatikanaji wa viongozi waadilifu watakaochaguliwa kuongoza nchi
kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Askofu Ayubu Mwakibinga amesema maombi hayo
hayakulenga tu kuliombea uchaguzi, bali pia kuombea umoja wa kitaifa, kuondoa
migawanyiko ya kisiasa na kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kubaki kuwa
kisiwa cha amani barani Afrika.
Askofu huyo pia amewaasa viongozi wa kisiasa kuweka
mbele maslahi ya Taifa na siyo maslahi binafsi au ya vyama vyao, huku akiwahimiza
wananchi kuendelea kushiriki kwa amani katika michakato yote ya uchaguzi.
Baadhi ya waumini waliohudhuria maombi hayo, akiwemo Bi.
Restuta Julius na Ndg. Mussa Ayubu, wameeleza furaha yao kwa namna kanisa hilo
limekuwa mstari wa mbele kuliombea Taifa ambapo wamesema maombi hayo
yamewajenga kiroho na kuimarisha mshikamano wao kama waumini na wananchi wa
Taifa la Tanzania.
Mfungo huu wa siku 38 umekuwa sehemu ya maandalizi ya kiroho kuelekea uchaguzi mkuu, ikiwa ni ishara ya mshikamano kati ya waumini na viongozi wa dini katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa nchi yenye amani, upendo na maendeleo endelevu.

Askofu Ayubu Mwakibinga akiongoza waumini wa Deliver
Hope Church of All Nations katika maombi maalumu ya mfungo wa siku 38 kuliombea
amani ya Taifa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, uliofanyika katika makao
makuu ya kanisa hilo yaliyopo Kijiji cha Nyanende, Kata ya Kizumbi, Manispaa ya
Shinyanga.

Askofu Ayubu Mwakibinga akiongoza waumini wa Deliver
Hope Church of All Nations katika maombi maalumu ya mfungo wa siku 38 kuliombea
amani ya Taifa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, uliofanyika katika makao
makuu ya kanisa hilo yaliyopo Kijiji cha Nyanende, Kata ya Kizumbi, Manispaa ya
Shinyanga.

Askofu Ayubu Mwakibinga akiongoza waumini wa Deliver
Hope Church of All Nations katika maombi maalumu ya mfungo wa siku 38 kuliombea
amani ya Taifa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, uliofanyika katika makao
makuu ya kanisa hilo yaliyopo Kijiji cha Nyanende, Kata ya Kizumbi, Manispaa ya
Shinyanga.
Mgeni rasmi, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Richard Makoye, akihutubia waumini na wageni waalikwa katika kilele cha maombi ya mfungo wa siku 38 yaliyoandaliwa na Deliver Hope Church of All Nations kwa ajili ya kuliombea amani ya Taifa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, uliofanyika katika Kijiji cha Nyanende, Kata ya Kizumbi, Manispaa ya Shinyanga.
Mgeni rasmi, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya
Shinyanga, Richard Makoye, akihutubia waumini na wageni waalikwa katika kilele
cha maombi ya mfungo wa siku 38 yaliyoandaliwa na Deliver Hope Church of All
Nations kwa ajili ya kuliombea amani ya Taifa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,
2025, uliofanyika katika Kijiji cha Nyanende, Kata ya Kizumbi, Manispaa ya
Shinyanga.

Baadhi ya waumini wa Deliver Hope Church of All
Nations, wakiungana katika maombi maalumu ya mfungo wa siku 38, wakiombea amani
ya Taifa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, yaliyofanyika katika makao makuu
ya kanisa hilo Kijiji cha Nyanende, Kata ya Kizumbi, Manispaa ya Shinyanga.

Post a Comment