Na Lydia Lugakila, Misalaba Media -Mbeya
Chifu George Lyoto kutoka kabila la Wasafwa Jimbo la Mbeya Mjini amewakilisha Machifu kwa kusema kuwa Patrick Mwalunenge ni mtu muhimu ambaye amekuwa akijihusisha na kusuluhisha migogoro mbalimbali katika jamii.
Chifu Lyoto ametoa kauli hiyo septemba 14, 2025 katika uzinduzi wa kampeini za Jimbo la Mbeya mjini.
Amesema Machifu wamemtuma kuwaelekeza wana Mbeya Mjini wajitokeze kwa wingi ili kutuma Mwalunenge kuwalete maendeleo.
Lyoto alisema, "Oktoba tukitiki tutakuwa tumepata mtu muhimu, huku akiahidi kuwa kundi hili la machifu halitamuangusha, bali limeisha mtunuku ushindi wa kishindo."
Kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa wazee wa CCM Isakwisa Stanton amesisitiza umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kukipatia ushindi chama hicho.
"Tarehe 29, tujitokeze zaidi tuweke tiki kwa mama Samia na kwa Mwalunenge pamoja na madiwani wetu," aliongeza Stanton.
Amesisitiza kuwa wana Mbeya wana bahati ya kwenda kupata "jembe la chuma" na hivyo Oktoba 29 ni lazima wampe mia kwa mia.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment