Madereva wanaoendesha bajaji katika Manispaa ya Shinyanga wamepewa elimu ya kuacha tabia ya kuzidisha abiria ili kuepuka kubeba abiria katika mazingira hatarishi na kuhakikisha usalama wa pande zote zinazohusika.
Akitoa elimu hiyo, Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, amewataka madereva hao kuacha mara moja tabia ya kuweka ubao kwenye kiti cha dereva na kubeba abiria zaidi ya idadi iliyokubaliwa.
Amesema tabia hiyo inaweza kusababisha ajali na hatari kwa abiria waliobebwa sehemu zisizo salama.
Sajenti Ndimila amewaasa madereva hao kufanya shughuli zao za usafirishaji kwa kufuata sheria za usalama barabarani bila kusubiri kushurutishwa au kusimamiwa. Alisisitiza kuwa madereva wanapaswa kuwa mabalozi wa usalama barabarani, kuonyesha mfano mzuri kwa watumiaji wengine wa barabara.
Elimu hii ni hatua muhimu ya kupunguza ajali zinazoweza kutokea kutokana na tabia ya kuzidisha abiria na kukuza utamaduni wa usalama barabarani katika Manispaa ya Shinyanga.“Kila dereva anapaswa kuhakikisha anaheshimu idadi ya abiria waliowekwa kwenye bajaji, kuepuka hatari na kuhakikisha abiria wanawasili salama,” alisema Sgt Ndimila.
Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, akiendelea kutoa elimu. 🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA


Post a Comment