Na Mapuli Kitina Misalaba
Katika kampeni zinazoendelea kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Mgombea
Ubunge wa Jimbo Jipya la Itwangi lililopo Mkoani Shinyanga kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Mhe. Azza Hillal Hamad, amejitokeza mbele ya wananchi na kuwaomba
kumpa kura za ndiyo ili aweze kuwatumikia kwa uadilifu na kuleta maendeleo ya
haraka katika jimbo hilo jipya.
Akizungumza na Misalaba Media wakati wa mkutano mkubwa
wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kishapu na mjini Shinyanga kwa lengo la kunadi sera na Ilani ya CCM, Azal Hilal amewashukuru
wananchi wa Itwangi kwa mapokezi makubwa na kuonyesha mshikamano wao na chama
hicho, akiwahimiza kuendeleza mshikamano huo kwa kujitokeza kwa wingi siku ya
uchaguzi.
“Naomba wananchi wenzangu wa Jimbo la
Itwangi mnipe kura za ndiyo ili niwe mwakilishi wenu bungeni. Pia naomba
tumuunge mkono kwa kura za ndiyo Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea
Mwenza Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ili tuhakikishe maendeleo yanaendelea kwa
kasi na nchi yetu inasonga mbele kwa mshikamano na amani,”
amesema Azza.
Azza Hillal amesisitiza kuwa ushindi wa pamoja kwa CCM
kuanzia nafasi ya Rais, Wabunge na Madiwani ni muhimu kwa utekelezaji wa Ilani
ya Uchaguzi ya 2025–2030 bila vikwazo, na kwamba wananchi wa Itwangi watapata
nafasi ya kushuhudia miradi mikubwa ya kimaendeleo ikitekelezwa kwa kasi katika
eneo lao.
Aidha, ameahidi kushirikiana kwa karibu na wananchi
mara baada ya kuchaguliwa, akiahidi kutetea maslahi ya wananchi wa Itwangi kwa
kuzingatia mahitaji ya sekta muhimu kama elimu, afya, barabara, maji safi na
salama, pamoja na fursa za ajira kwa vijana.
Mgombea Ubunge wa Jimbo Jipya la Itwangi lililopo Mkoani Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Azza Hillal Hamad, akizungumza.
Mgombea Ubunge wa Jimbo Jipya la Itwangi lililopo Mkoani Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Azza Hillal Hamad, akizungumza.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment