" MWALUNENGE AAHIDI KUFANYA MAKUBWA KWA WANANCHI KATA YA NZOVWE MKOANI MBEYA

MWALUNENGE AAHIDI KUFANYA MAKUBWA KWA WANANCHI KATA YA NZOVWE MKOANI MBEYA

Na Lydia Lugakila 

Mgombea ubunge Jimbo la Mbeya mjini kupitia tiketi ya chama mapinduzi CCM Mhe, Patrick Mwalunenge ameahidi kuwaleta maendeleo wananchi wa kata ya Nzovwe Mkoani Mbeya huku akisisitiza kufanya kazi bila kuchoka akitumia ubunifu na maarifa.

Mwalunenge ametoa kauli hiyo Septemba 3, 2025 wakati alipofika katika kata ya Nzovwe kwa ajili ya kutoa shukrani kwa wananchi, wajumbe na viongozi wote wa chama waliomchagua kwa kura za kishindo kati ya wagombea sita wa chama hicho waliokuwa wakiomba ridhaa ya kugombea ubunge wa Jimbo la Mbeya mjini.

Mgombea huyo amesema kuwa kwa sasa ana deni kubwa la kuwafanyia kazi wananzovwe ambapo amewaomba wamtume Bungeni ili awaletee maendeleo kwani atahakikisha anafanya kazi kwa ubunifu na kuwajali wananchi bila kujali itikadi zao.

"Naomba mnitume maana nyinyi ndo mabosi wangu ndio mlionipigia kura nikawa mshindi hivyo ili yale mnayotamani yatokee kwenye kata hii basi lazima muamue"alisema Mwalunenge.

Amesema kuwa wananchi wategemee mambo makubwa huku akiwahimiza kushikamana kwani bila upendo maendeleo hayawezi kuja.

"Kumbukeni kwenye fitina na vurugu maendeleo hayawezi kuja"alisema kiongozi huyo.

Amewaomba wananchi wa chama hicho kuhakikisha Oktoba 29,2025 wanajitokeza kwa wingi kupiga kura ili wakiletee ushindi chama hicho kwa kumchagua mbunge Diwani na Rais ili kutimiza malengo waliyojiwekea.

Aidha amesema kuwa ataendelea kuwasaidia wananchi wake kwani amekuwa akijitoa kwa kusaidia watu mbali mbali bila ubaguzi ambapo tayari amefanikisha kutoa zaidi ya shilingi milioni 150 kanisani kupitia harambee huku akiahidi kuleta miradi mipya na kufufua iliyolala edapo akafanikiwa.

Kwa upande mgombea udiwani wa kata ya Nzovwe Bwn Leo Mwakapila ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM katani humo amempongeza mgombea ubunge huyo kwa huruma yake ya kuwasaidia watu mbali mbali kwani imekuwa ni kawaida yake.

Hata hivyo katibu wa CCM kata ya Nzovwe Sebha Mussa amesema mshikamano upendo na umoja ndio nguzo muhimu katika kuleta ushindi wa chama hicho huku akiwashukuru wananchi wa kata hiyo waliompigia kura na kumfanya anakisaka kitu hicho cha ubunge kwa sasa ambapo ameahidi ushirikiano kati yake na mgombea ubunge ili wafanikishe ushindi wa kishindo kwa Rais Samia.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post