Madereva wa pikipiki wanaosafirisha abiria nyakati za usiku katika Manispaa ya Shinyanga wamepewa elimu ya usalama barabarani kwa lengo la kuwakinga na ajali zinazoweza kuepukika endapo watachukua tahadhari.Elimu hiyo imetolewa na Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, ambaye amewasisitiza madereva hao kuacha mara moja shughuli za usafirishaji wa abiria pale wanapopatwa na usingizi na badala yake waende kupumzika kabla ya kuendelea na safari.Sajenti Ndimila amesema uchovu na usingizi ni miongoni mwa sababu kubwa za ajali kwa madereva wa pikipiki kwani hali hiyo huwafanya washindwe kumudu vyema usukani na kupoteza mwelekeo barabarani, jambo linaloweza kusababisha madhara makubwa kwao na abiria wanaowasafirisha.Aidha, amewataka madereva hao kujali usalama wa maisha yao na ya abiria kwa kuepuka tamaa ya fedha wakati wakiwa wamechoka, huku akisisitiza kuwa kuendesha chombo cha moto bila utimamu wa mwili na akili ni hatari na kunahatarisha maisha ya watu wengi.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment