Na Lydia Lugakila, Misalaba Media -MbeyaKatika tukio la kihistoria, wananchi wa jimbo la Mbeya mjini wamejumuika kwa wingi kumsikiliza mgombea ubunge kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Patrick Mwalunenge katika Uzinduzi wa kampeni yake uliofanyika katika eneo Kabwe, Septemba 14,2025,ambapo shangwe na nderemo zilitawala huku wengine wakieleza kuwa kuoekana kwa mvi katika kichwa cha mgombea huyo tayari Wananchi hao wanakwenda kupona endapo watamchagua kupeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya Ubunge.Wananchi hao walionyesha hisia kubwa na shauku ya kusikia kutoka kwa mgombea wao, ambapo miongoni mwa maneno yaliyotawala yalikuwa ni "ukiona mvi zinamelemeta ujue Mbeya tumepona". Kauli hizo zilionyesha kuamuamini Mwalunenge na kuwa na matumaini ya maendeleo chini ya utawala wa CCM.Pamoja na kuhudhuria viongozi mbalimbali, wakazi wa Mbeya wamesisitiza kuwa ushindi wa chama hicho tayari umehakikishwa huku wakimpongeza Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi cha miaka mitano na kuonesha matumaini makubwa katika mwelekeo wa mbeleni.Hali hiyo kwa wananchi ilikuwa na maana kubwa si tu kwa CCM bali kwa maendeleo ya jimbo zima la Mbeya mjini. Wananchi wamejitokeza kwa umati mkubwa, wakionyesha ujasiri na hali ya kuunga mkono kampeni hiyo, huku wakitarajia mabadiliko chanya na maendeleo endelevu chini ya uongozi wa Patrick Mwalunenge.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment