Waongoza wanyama wanaotumia mikokoteni katika Wilaya ya Shinyanga wamepewa elimu ya usalama barabarani ili kuwaepusha na ajali wanapotekeleza majukumu yao.
Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga, Koplo Shafii Mbinga, ambaye amewataka kuhakikisha hawatumii wanyama wenye uoni hafifu na badala yake kuwaongoza upande sahihi wa barabara ili kuepusha ajali.
Koplo Mbinga amewasisitiza pia kuwa mabalozi wa usalama barabarani kwa kuwafikishia elimu hiyo watu wengine wanaojihusisha na kazi kama hiyo, ili kuhakikisha kila mmoja anakuwa salama anapokuwa barabarani.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment