Na Alphonce Kapela - Misalaba Media Wazazi wenye watoto wanaosoma shule ya Victoria Hope Nursery and Primary School iliyopo Buhongwa Mwanza wameombwa kushirikiana na uongozi wa shule Ili kufikia Malengo ya watoto wanaosoma shuleni hapo.Akizungumza katika Mahafali ya Kwanza ya shule hiyo Meneja wa CRDB tawi la Buhongwa ambae alikuwa mgeni rasimi katika Mahafali hayo Grace Anthony amesema bila ushirikiano kati ya Wazazi na uongozi wa shule watoto wanaweza wasifanye vizuri."Mimi niwaombe Wazazi muendelee kushirikiana na uongozi wa shule Kwa kutoa maoni ya kujenga Ili shule iweze kupiga hatua"alisema GraceIli kuunga mkono juhudi zinazofanywa na shule ya Victoria Hope Nursery and Primary Meneja wa CRDB tawi la Buhongwa amesema watawapatia Kompyuta,Vitabu na Vifaa vya kufundishia.Kwa upande wake mthibitiubora wa shule mkuu wilaya ya Misungwi Mwl Fautine Salala amempongeza mkurugenzi wa shule ya Victoria Hope Nursery and Primary School Kwa uwekezaji mkubwa alioufanya unaoendana na vigezo vinavyotakiwa na serikali."Kwa namna nilivyoona kile ambacho watoto wamefanya hapa nimeona namna Walimu walivyowekeza Kwa watoto na ndio maana wanafanya vizuri"alisema SalalaNae Mzazi Magreth Willyfredy ameupongeza wa Victoria Hope Nursery and Primary School Kwa kufanikisha Mahafali ya Kwanza Kwa mwaka huu 2025 na kuwatakia Kila la heri watoto wanaotarajia kufanya mtihani wao wa darasa la Saba hivi karibuni.Jumla ya wanafunzi tayajali 16 ambapo Wasichana ni wawili na wavulana 14 watarajiwa kufanya mtihani wa darasa la Saba mwaka huu

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment