" ZAIDI YA DOLA BILIONI 2 ZINAHITAJIKA KUTEKELEZA MKAKATI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA AFTIKA

ZAIDI YA DOLA BILIONI 2 ZINAHITAJIKA KUTEKELEZA MKAKATI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA AFTIKA






Pembezoni mwa Mkutano wa Pili wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Afrika kuhusu Tabianchi jijini Addis Ababa, Ethiopia, viongozi na wadau mbalimbali wa nishati safi ya kupikia Afrika, ikiwemo Tanzania wamekutana kujadili mbinu na mahitaji mbalimbali ya Bara la Afrika katika kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Akifungua mjadala wa Mkakati wa Nishati Safi ya Kupika Barani Afrika: Kuongeza Usuluhishi Endelevu, Ufadhili, na Ubia katika Upatikanaji wa nishati safi, kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika uwekezaji, ufadhili wa masharti nafuu, ubunifu, teknolojia za kisasa na rafiki, kubadilishana ujuzi na miundombinu itayowezesha kutimiza malengo ya kitaifa na kimataifa.

Changamoto zitokanazo na matumizi ya nishati chafu zinaleta jitihada za pamoja za Serikali za Afrika, taasisi za kifedha, mashirika binafsi na wafadhili kutafuta zaidi ya dola bilioni mbili kila mwaka zitakazochangia kuleta suluhu.

Washiriki wa mjadala huo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa jitihada za nishati safi ya kupikia. Mkakati wa Tanzania katika kuhakikisha 80% ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034 unajumuisha matumizi ya umeme, gesi asilia, LPG, teknolojia za upepo, jua na biomasi bunifu, hatua inayolenga kuboresha afya, kulinda mazingira na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa.

Mjadala huu ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhandisi Cyprian Luhemeja; Waziri wa Mazingira, Tabianchi na Wanyamapori wa Zimbabwe, Evelyn Ndlovu; Waziri wa Nchi Nishati na Madini kutoka Uganda, Mhe. Phiona Nyamutoro; wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, wawakilishi kutoka CRDB, pamoja na wadau wa nishati safi kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA



Post a Comment

Previous Post Next Post