" WANAWAKE WATATU NA MUME WAO WAHAMIA CCM KUTOKA CUF KILWA

WANAWAKE WATATU NA MUME WAO WAHAMIA CCM KUTOKA CUF KILWA


Na Osama Chobo, Misalaba Media -kilwaWanawake watatu pamoja na mume wao wamehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakitokea Chama cha Wananchi (CUF) katika kijiji cha Pungutini, kata ya Kinjumbi, wilayani Kilwa, mkoani Lindi, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni za CCM zinazofanyika katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Kilwa Kaskazini.Akizungumza kwa niaba ya wake zake, aliyekuwa Mwenyekiti wa zamani wa CUF kata ya Kinjumbi, Ndugu Saidi Kaonene, alisema kuwa uamuzi wao wa kujiunga na CCM umetokana na imani waliyoipata kutokana na utendaji kazi mzuri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake. “Hakuna mtu aliyenishawishi kujiunga na CCM, bali ni mambo mazuri na kazi kubwa anazofanya Dkt. Samia kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania. Mimi na familia yangu tumeona ni busara kuungana na wananchi wengine wa Pungutini kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita,” alisema Kaonene.Aliongeza kuwa yeye pamoja na wake zake watatu wameamua kushirikiana na wananchi wa eneo hilo kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika uchaguzi ujao ili kuendelea kuleta maendeleo katika jamii yao.Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia CCM, Mheshimiwa Kinjekitile Ngombale Mwiru, aliwakaribisha wanachama hao wapya na kuwahakikishia kuwa chama hicho kimejipanga kuhakikisha wananchi wote wanapata maendeleo ya kweli.> “Tumekuja kufanya kazi kwa ajili ya wananchi. Naomba mnipatie kura zenu ili tuweze kusonga mbele kwa maendeleo. Maendeleo yanakuja, tushirikiane kuyakaribisha,” alisema Mh. Ngombale Mwiru.Alihitimisha kwa kuwashukuru wananchi wote waliohudhuria mkutano huo wa kampeni na kuahidi kuwa endapo watampa ridhaa ya kuwa mbunge wao Oktoba 29, atahakikisha anaendelea kuwaletea maendeleo kwa vitendoMgombea Ubunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia CCM, Mheshimiwa Kinjekitile Ngombale Mwiru.


Post a Comment

Previous Post Next Post