Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kupinga Ukatili Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA), Shujaa Sospeter Bulugu, ametangaza rasmi uteuzi mpya ndani ya uongozi wa taifa.
Katika taarifa hiyo, Shujaa Sospeter amemteua Daniel Kapaya kuwa Mkuu wa Idara ya Makongamano, Utamaduni na Utalii—SMAUJATA Taifa. Uteuzi huu unamfanya Kapaya kushika jukumu hilo muhimu katika kusimamia na kuratibu shughuli zote za makongamano, kukuza utamaduni na kuendeleza sekta ya utalii ndani ya jumuiya hiyo.
Aidha, kabla ya uteuzi huo Daniel Kapaya alikuwa Katibu wa SMAUJATA Kanda ya Ziwa, pia aliwahi kutumikia nafasi ya katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga na kwa sasa atabaki na nafasi yaje hiyo ya kitaifa.
Uteuzi huu unalenga kuimarisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika harakati za kupinga ukatili na kuhamasisha maendeleo ya jamii kupitia makongamano, utamaduni na utalii.

Post a Comment