Na Lydia Lugakila, Misalaba Media - MbeyaBi Joyce Yosam Mwampamba amewataka wazazi kuongeza ukaribu na watoto wao ili kutambua kwa urahisi vitendo vya ukatili wanavyoweza kukabiliana navyo, ikiwemo matukio ya ulawiti.Amesema hayo alipohudhuria kama mgeni rasmi katika mahafali ya Shule ya Lwekebu Day Care iliyopo Iwambi, mkoani Mbeya.Amesema kuwa baadhi ya wazazi wameshindwa kuwalea watoto ipasavyo kutokana na majukumu ya kutafuta pesa, hali inayowafanya kukosa muda wa kuzungumza na watoto wao.Amesisitiza kuwa ukosefu huo wa mawasiliano unachangia watoto kukutana na matukio mbalimbali ya ukatili bila wazazi kutambua kwa wakati."Wazazi leo wameshindwa kuwalea watoto vizuri kutokana na kuwa bize kupitiliza katika kutafuta pesa, na hawana muda wa kukaa na watoto wao ambapo hali hii inasababisha watoto kukutana na matukio ya ukatili,” alisema Bi Josam.Aidha, amewahimiza wazazi kuandaa mazingira rafiki yatakayowajenga watoto kupenda masomo, ikiwa ni pamoja na kuwapa motisha pale wanapofanya vizuri. Ameongeza kuwa wazazi wanapaswa kuwapa watoto uhuru wa kujieleza ili waweze kufichua mambo mazuri na mabaya wanayokutana nayo.Bi Joyce amewaomba wazazi kujiepusha na tabia zisizofaa nyumbani, ikiwemo kutumia lugha za matusi na kuwa wakali kupitiliza ambapo amesema kuwa wazazi wanapaswa kuwa walezi wazuri ili kuwapunguzia walimu mzigo wa malezi shuleni.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment