" MACHAFUKO DAR ES SALAAM: TASNIA YA HABARI YAGAWANYIKA JUU YA KIINI HALISI

MACHAFUKO DAR ES SALAAM: TASNIA YA HABARI YAGAWANYIKA JUU YA KIINI HALISI

Kipindi cha ghasia na vurugu kilichotikisa jiji la Dar es Salaam kati ya Oktoba 29 na Novemba 1, 2025, kimeibua mgawanyiko mkali ndani ya tasnia ya habari na uchambuzi nchini. Huku wengine wakikemea uhalifu na uporaji, wengine wanasisitiza kuwa matukio hayo ni matokeo ya ukosefu wa haki na mfumo.

Taarifa za kiintelijensia kuhusu uwezekano wa ghasia zilikwishathibitika baada ya "maandamano ya amani" kugeuka haraka kuwa vitendo vya uhalifu. Ndani ya dakika chache, hasara kubwa ilitokea, ikijumuisha:Vituo viwili vya BRT vilichomwa,Basi moja la mwendokasi liliharibiwa vibaya na

Vituo vya mafuta na maduka ya wananchi viliteketezwa au kuharibiwa.

Mchambuzi Benjamin Thompson katika kundi sogozi la Tasnia alikosoa vikali waliokiuka amri halali ya kutotembea (curfew), akisisitiza kuwa ilikuwa ni "sababu ya ujinga tu" kuongelea haki za kikatiba "wakati watu tuko vitani."

Malumbano ya Tasnia: Haki, Njaa na 'Moto Rafiki'

Katika majukwaa ya wachambuzi, malumbano makali yalijitokeza juu ya kiini halisi cha matatizo na namna ya kuyashughulikia:

Mchambuzi Ahmad Mmow alilaani uporaji lakini akashikilia msimamo kuwa matukio haya ni matokeo ya kukosa busara na kuhurumiana, akisisitiza kuwa wahanga wengine waliouawa walikuwa raia wasio na hatia.

“Huyo aliyeuwawa akiuza supu sio mhalifu bali njaa ilimfanya abahatishe ili apate riziki,” alisema Mmow. Kauli hii iliungwa mkono na Deus Mhagale aliyesisitiza kuwa: "Amani bila haki hakuna kitu."

Utata wa 'Friendly Fire'

Mwandishi Derek Murusuri alipongeza vikosi vya ulinzi kwa "kuweka rekodi Afrika ya kumaliza machafuko yenye sura ya ugaidi ndani ya siku mbili tu," lakini aligusia suala la raia kupoteza maisha kwa "bahati mbaya, ambao jeshini tulikuwa tunaita, friendly fire."

Kauli hii ya "madhara madogo" ilipingwa vikali na Mmow, ambaye alihoji: "Mlitaka wafe watu wangapi, miundombinu kiasi gani iharibiwe... mpaka mseme madhara ni kidogo?"

Mchambuzi mitumba2005 alipendekeza Katiba mpya na kubadili mfumo wa upatikanaji wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kama suluhisho la kudumu.

Sauti nyingine ilipinga wito wa Katiba Mpya, ikisisitiza kuwa shida si Katiba, bali ni kutotekelezwa kwa Katiba ya 1977 na kukosekana kwa utawanyaji wa mamlaka kwa kufuata utamaduni wa nchi. Hoja ilikuwa: "Kujidanganya kwa kuimba wimbo wa Katiba Mpya wakati tulichonacho hakijatumika, ni kuchelewesha maendeleo na kuvuruga uchumi."

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA


Post a Comment

Previous Post Next Post