
Mhe. Mussa Azzan Zungu Spika mpya wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungnao wa Tanzania.
Zungu amechaguliwa kushika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Spika wa bunge hilo, Dkt. Tulia ackson, kutangaza kujiondoa katika mbio za kugombea Uspika wa bunge.
Zungu ambaye ni mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es salaam kupitia Chama cha Mapinduzi CCM alikuwa ni miongoni wa wagombea 6 waliojitokeza kugombea nafasi hiyo,ambapo yeye pekee alikuwa anatoka bungeni na wagombea 5 wametoka nje ya bunge wakiwakilisha vyama vingine vya siasa.
Zungu amechaguliwa kwa kura 378 kati ya 383 zilizopigwa kutoka kwa wabunge wa bunge la Tanzania, huku kura 3 zikiharibika.
Post a Comment