
Chama cha ACT-Wazalendo kimeanza rasmi mchakato wa kisheria kudai haki za baadhi ya wawakilishi wake wanaodai kuporwa ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.
Kesi hizo zitaanza kutajwa leo tarehe 10 Disember 2025 saa tatu kamili za asubuhi katika Mahakama Kuu ya Zanzibar iliyopo Tunguu, katika hatua ambayo ACT-Wazalendo inaieleza kuwa ni sehemu ya mapambano yake ya kudai haki na kuleta uwazi katika mchakato wa uchaguzi.
Kwa mujibu wa kauli za viongozi wa chama hicho, uchaguzi wa mwaka 2025 uligubikwa na ubadhirifu na ukiukwaji wa taratibu, hasa katika maeneo ambayo chama kinadai kuwa kilishinda lakini matokeo yakabadilishwa kinyume cha sheria.
ACT-Wazalendo imeeleza kuwa itaendelea kufuata njia za kisheria ili kuhakikisha wawakilishi wanaodaiwa kuporwa ushindi wanarejeshewa haki yao.
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment