
Msanii maarufu wa muziki Afro-pop, wenye ladha ya kibongofleva Christian Bella Obama (CBO) hatimaye amepewa Uraia wa Tanzania baada ya kuishi kwa miaka zaidi ya 20 akifanya muziki hapa nchini.
Bella alikuja Tanzania akiwa na umri wa miaka 17 mpaka sasa ana miaka zaidi ya 30 akizungumza na ripota wa @ayotv_ Vido Vidox amesema “Ninamshukuru Mungu Nashukuru Serikali ya Tanzania na Watanzania kwa ujumla, Watanzania wananipenda na Watanzania ndio wamenibeba nina miaka 20 ndani ya Tanzania niliingia nikiwa na miaka 17 nilikuwa chini ya umri wa miaka 18.”
“Kufanya kazi nchi ambayo haujazaliwa sio kazi ndogo lakini nimekuja nikiwa mdogo nimepokelewa vizuri kitu inaonesha napendwa sana sihitaji kuwa na nyimbo mpya ili kupewa kazi napata kazi sana kuliko wasanii waliopo kwenye trending”
“Sijapewa uraia kwa sababu nina Watoto na Mtanzania ni mchakato mrefu sana na lazima kuzifuata hata kama unapendwa na viongozi nilifuata utaratibu sio Kwamba Bella kapewa kirahisi na utaratibu sio mrahisi ni kazi ndefu sana inaanzia serikali za mitaa unakuja Wilayani unaenda kwa Mkuu Mkoa, kuna vitu vingi na ukiwa mgeni lazima uoneshe ulikuwa unaishi halali na hawatoi Uraia Sababu Bella unaimba vizuri Hapana hata ukifanya miaka 40, lazima ufuate utaratibu nimekaguliwa vitu vingi sana kuna Polisi na vitu vingi sana” Amesema Christani Bella
Aidha Uraia wa Bella umetangazwa Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene leo Alhamisi, Desemba 18, 2025 ikiwa ni siku ya wahamaji duniani ambapo Waziri Simbachawene amesema Tanzania kuna idadi kubwa ya wahamiaji na baadhi yao wamekuwa wakipewa uraia
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment