Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho, Jenista Joakim Mhagama, kilichotokea leo Alhamisi Desemba 11, 2025, jijini Dodoma.“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho Mheshimiwa Jenista Mhagama kilichotokea leo 11 Desemba, 2025 jijini Dodoma.
Natoa pole kwa waheshimiwa Wabunge wote, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Peramiho. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” ameeleza Spika Zungu kupitia taarifa hiyo.
Mhagama, aliyekuwa mbunge na kiongozi mwenye mchango mkubwa katika utumishi wa umma, alizaliwa Juni 23, 1967 na amehudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya Serikali na Bunge la Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ofisi ya Bunge inashirikiana na familia ya marehemu kuratibu taratibu za mazishi na taarifa zaidi zitatolewa kadiri mipango itakavyokamilika.
“Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, amina,” imeeleza taarifa hiyo.
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment