" MISRI YATINGA HATUA YA 16 BORA AFCON 2025

MISRI YATINGA HATUA YA 16 BORA AFCON 2025











Timu ya Taifa ya Misri imefanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora ya michuano ya Mataifa ya Afrika AFCON 2025, baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Afrika Kusini katika mchezo uliopigwa leo, Desemba 26, 2025, nchini Morocco.

Kufuatia ushindi huo, Misri wanakuwa timu ya kwanza katika Kundi B kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo, baada ya kufikisha pointi 6.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na nahodha Mohamed Salah dakika ya 45+1, kwa mkwaju wa penalti.



Awali Angola waliminyana na Zimbabwe ambapo walitoka sare ya bao moja kwa moja.

Mchezo wa mwisho wa kundi hilo Afrika ya Kusini watacheza na Zimbabwe, huku Angalo wakiminyana Misri.


Post a Comment

Previous Post Next Post