Na Lydia Lugakila, Misalaba Media - Bukoba
Lake Zone Driving School, iliyopo Bukoba mkoani Kagera, imeendelea kuwa miongoni mwa vituo vinavyoongoza kwa kutoa mafunzo bora na ya kisasa ya udereva kwa wanafunzi wa rika zote.
Akizungumza na Misalaba Media, Mkurugenzi wa kituo hicho Winston Kabantega amesema kuwa shule hiyo inatoa mafunzo ya kuendesha magari ya gia (Manual) pamoja na magari ya gia (Automatic), huduma zinazotolewa na wakufunzi wenye uzoefu mkubwa na mbinu bora za ufundishaji.
Kabantega amesema kuwa baada ya mwanafunzi kukamilisha mafunzo na taratibu zote, kituo husaidia kuongeza ufanisi katika mchakato wa kupata leseni kwa haraka, kupitia mfumo wa kujihudumia wa TRA.
"Tunasaidia pia mwanafunzi au dereva aliye poteza leseni kuipata tena kupitia mfumo na kwa yule asiye na cheti tunamfundisha kwa utaratibu maalum hadi afuzu na kupata cheti chake,” amesema Kabantega.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa kituo hicho kinatoa fursa kwa wanafunzi kusoma kulingana na ratiba zao binafsi, jambo linalowanufaisha zaidi wafanyakazi, akina mama wa nyumbani na watu wengine wenye majukumu mengi.
Ameongeza kuwa huduma nyingine zinazotolewa ni pamoja na Mafunzo ya utangulizi wa kompyuta (Computer Introduction),
Vitabu vya alama na sheria za usalama barabarani kwa bei nafuu,cheti cha udereva kinachowekwa kwenye mfumo mara baada ya kuhitimu
Amewasihi Wananchi wa Mkoani Kagera na Tanzania kwa ujumla kuzitembelea Ofisi za Lake Zone Driving School zinazopatikana Bukoba mjini, karibu na Polisi Canteen, barabara iendayo tawi la NMB Kaitaba Ili kuvuna maarifa.
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment