
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema limepata changamoto kwenye mfumo wa umeme karibu na Stesheni ya Ruvu mkoani Pwani, hali iliyosababishwa na mvua inayoendelea kunyesha nchini.
Akizungumza na Swahili Times, Afisa Habari wa TRC, Fred Mwanjala amesema kwa sasa mafundi wako eneo la tukio kuhakikisha wanarejesha miundombinu ili huduma za usafiri zirejee kama kawaida.
“Napenda kuwaomba radhi abiria wetu kwa changamoto iliyojitokeza, hilo ni suala ambalo huwezi kuliepuka ni suala la kiufundi,” amesema Mwanjala.
Shirika hilo limewashukuru Watanzania kwa kuwa wavumilivu nyakati zote.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment