" PROF. SHEMDOE ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA MIRADI JIJINI ARUSHA.

PROF. SHEMDOE ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA MIRADI JIJINI ARUSHA.

Na, Egidia Vedasto, 

Misalaba Media, Arusha. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe ameridhishwa na hatua za ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Jijini Arusha.


Profesa Shemdoe amefanya ukaguzi huo Leo jijini Arusha  akiambatana na Meya wa Jiji la Arusha Maxmillian Iranqhe ambapo katika mazungumzo yake amesisitiza miradi hiyo kukamilika mapema iwezekenavyo mwaka ujao. 

"Ujenzi wa soko la kilombero na stendi ya bondeni vinatakiwa kukamilika mwezi May 2026 sambamba na uwanja wa mpira unatakiwa kukamilika November 2026 ili kufanya maandalizi ya mashindano ya AFCON mwaka 2027, wananchi wana kiu ya maendeleo na wanataka mabadiliko ya haraka"amesema Prof.Shemdoe. 

Katika namna hiyo hiyo Meya wa Jiji la Arusha Maxmillian Iranqhe amesema  wamepokea maelekezo hayo na watahakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kama inavyotakiwa. 

"Kipekee tunamshukuru Mheshimiwa Waziri kututembelea, tuna imani naye na tunamshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha za miradi ya maendeleo  tunawahakikishia wananchi tutatimiza adhma hiyo, nawaahidi wananchi mambo mazuri yanakuja" Amesema Iranqhe.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post