
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi na Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kabla ya kufungua mkutano wa 9 wa CDF na Makamanda uliofanyika katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) mkoani Tanga tarehe 15 Desemba 2025.

Matukio mbalimbali wakati wa Mkutano wa 9 wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Makamanda uliofanyika katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) mkoani Tanga. Mkutano huo wa CDF na Makamanda ulifunguliwa na rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 15 Desemba, 2025.
………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan amefungua rasmi Mkutano wa 09 wa CDF na Makamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania unaofanyika katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga iliyopo Mkoani Tanga leo tarehe 15 Disemba 2025.
Akizungumza na Makamanda, Mheshimiwa Rais amelipongeza JWTZ kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa kwa kuhakikisha Taifa liko salama wakati wote. Amewahakikishia Makamanda kuwa Serikali itaendelea kuliwezesha JWTZ kwenye kila Nyanja ikiwemo zana, vifaa, Miundombinu na Mafunzo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa utulivu.
Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa namna Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuliwezesha JWTZ kutekeleza majukumu yake. Amemhakikishia kuwa Jeshi litaendelea kulinda mipaka ya nchi na watu wake dhidi ya matishio yoyote yatakayojitokeza .
Mkutano wa CDF na Makamanda wa JWTZ ni jukwaa lililoanzishwa na Mkuu wa Majeshi likiwa na lengo la kuwakutanisha Makamanda ili kupata wasaa wa kujadiliana maswala mbalimbali ya Ulinzi kwa maslahi ya Taifa.



Matukio mbalimbali wakati wa mkutano wa 9 wa CDF na Makamanda uliofanyika katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) mkoani Tanga. Mkutano huo wa CDF na Makamanda ulifunguliwa na rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 15 Desemba 2025.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment