" SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UNUNUZI WA JAS CHINI YA BEI ELEKEZI SAME

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UNUNUZI WA JAS CHINI YA BEI ELEKEZI SAME






Na Ashrack Miraji 

Serikali kupitia Wizara ya Madini imepiga marufuku ununuzi wa madini ya jasi chini ya bei elekezi iliyotolewa na Tume ya Madini katika eneo la Makanya wilayani Same, mkoani Kilimanjaro, huku ikiwataka wanunuzi wote kuzingatia miongozo hiyo ili kulinda maslahi na ustawi wa wachimbaji wadogo wa madini hayo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uchimbaji wa madini ya jasi wilayani Same, ambapo pia alizungumza na wachimbaji wadogo na kusisitiza umuhimu wa kurejesha mazingira kwa kufukia mashimo mara baada ya kukamilika kwa shughuli za uchimbaji.

Dkt. Kiruswa pia amebainisha fursa mbalimbali zilizopo kwa vijana na wanawake katika Sekta ya Madini kupitia programu ya Mining for a Brighter Tomorrow (MBT), akiwahimiza kuchangamkia mafunzo, upatikanaji wa leseni na matumizi ya vifaa vya kisasa ili kuongeza tija na usalama katika uchimbaji wa madini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni amesema Serikali itaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria, kanuni na miongozo ya madini ili kuhakikisha wachimbaji wadogo na wananchi wa maeneo husika wananufaika na rasilimali hiyo kwa kukuza uchumi wao.

Naye Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Abel Madaha, amesema Tume ya Madini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikifanya vikao mara kwa mara kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji kuanzia migodini hadi masoko ya madini.

Pamoja na hayo, Naibu Waziri wa Madini amesema Serikali inapanga kuwakutanisha wadau wa madini ya jasi mwanzoni mwa mwezi wa kwanza jijini Dodoma ili kujadili changamoto zinazowakabili wachimbaji wa Mkoa wa Kilimanjaro na kutafuta suluhu ya kudumu.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post