Katika hali inayoashiria kuongezeka kwa umakini wa Serikali dhidi ya mbinu mpya za "Wababe wa dunia" wanaotafuta kuvuruga mataifa yanayochipukia, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa onyo kali kuhusu mtego wa kidini unaosukwa kuhujumu amani ya nchi.
Akizungumza Desemba 29, 2025, wakati wa ziara ya kikazi jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amechambua kwa kina namna mataifa mengi yanavyoingizwa kwenye machafuko kupitia mbinu za kupandikiza chuki za kiimani.
Waziri Mkuu amebainisha kuwa Tanzania imefanikiwa kuvuka mtego wa ukabila uliolimaliza mataifa mengine, lakini sasa kuna jitihada za makusudi za kutaka kuitumbukiza nchi kwenye mtego wa udini—mtego ambao ameuita kuwa "hauna mshindi."
Tofauti na migogoro mingine, mgogoro wa kidini unagusa hisia za ndani kabisa za binadamu. "Ukigusa imani ya mtu, hapo hakuna mshindi," alionya Waziri Mkuu, akisisitiza kuwa moto wa kidini ukishawaka, hauchagui mchochezi wala mnyamazaji.
Mkakati wa 'Gawa Uwatawale':
Katika muktadha wa kimataifa, kuna mbinu zinazotumiwa na "wababaishaji wa dunia" kudhoofisha mataifa yenye rasilimali kwa kuchochea migawanyiko ya ndani. Udini unatajwa kuwa njia rahisi inayotumiwa sasa kuifanya Tanzania ipoteze uelekeo wa maendeleo.
Kutokana na mazingira hayo alisema Waziri Mkuu falsafa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya maridhiano na mazungumzo (R4) ndiyo kinga pekee. Viongozi wa dini na siasa wamehimizwa kutumia milango iliyo wazi ya Serikali kuwasilisha hoja zao badala ya kushambuliana hadharani.
Uhusiano wa Amani na Utulivu wa Sasa
Kauli hii imekuja wakati mwafaka ambapo Tanzania inajipanga kwa ajili ya hatua kubwa za kimaendeleo. Waziri Mkuu ameweka msisitizo kuwa Serikali haina dini, lakini ina jukumu la kikatiba la kulinda uhuru wa kila mwananchi kuabudu. Huu ndio msingi mkuu wa amani ya Tanzania. Amewataka Watanzania kuwa macho na mitego inayolenga kuwagawa, wakikumbushwa kuwa umoja wao ndio nguvu inayozuia harakati za wababaishaji wa kimataifa.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment