" JESHI LA ZIMAMOTO RUVUMA LAKARIBISHA ASKARI WAPYA NA KUTUNUKU VYETI VYA PONGEZI KWA ASKARI BORA WA MWAKA

JESHI LA ZIMAMOTO RUVUMA LAKARIBISHA ASKARI WAPYA NA KUTUNUKU VYETI VYA PONGEZI KWA ASKARI BORA WA MWAKA


 Na Osama Mohamedi chobo, Misalaba Media -Songea

Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Ruvuma lafanya ghafla  kusheherekea mwaka mpya kwa kuwakaribisha askari wapya na kutoa tuzo ya pongezi kwa Askari bora wa mwaka ambapo katika ghafla hiyo ilofanyika  tarehe 2/1/2026 kwenye viwanja vya jeshi hilo lililopo kata ya misufini Manispaa ya songea 

Akizungumza katika hafla hiyo fupi Mrakibu Mwandamizi  ambaye ni kaimu kamanda Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ruvuma Melania B. Nyabwinyo amewashukuru maafisa na Askari kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kuokoa maisha na mali za watanzania licha ya changamoto mbalimbali wanazokutana nazo 

Pia ameelezea namna ya jeshi hilo lilivyojipanga kuhakikisha wanaweza kuzuia majanga yasitokee kwa kuhakikisha wanafanya ukaguzi na kutoa elimu ya tahadhari dhidi ya majanga ya moto ili kutimiza malengo ya jeshi kwa mwaka 2026

Kwa upande mwingine konstebo Leonard vicent mgaya ameibuka mshindi na kupokea pongezi kutoka kwa mgeni rasmi ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wake katika utekelezaji wa majukumu.

Akizungumza baada ya kupokea pongezi hiyo konstebo Leonard amewashukuru maafisa na Askari wote kwa ushirkiano wao kwani bila ushirkiano wa wote hakuna ufanisi wa kazi.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post