Na. Elias Gamaya – Nzega, Tabora
Mbunge wa Jimbo la Bukene, Mhe. John Stephano Luhende, kwa
kushirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, Rtd SSP Aron
Maganga, imetembelea na kuwafariji wahanga wa kimbunga kilichosababisha
uharibifu mkubwa wa makazi katika Kata ya Kasela, Kijiji cha Nindo, Kitongoji
cha Kaselya.
Aidha, Ofisi ya Mbunge imetoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti, kuepuka ukataji ovyo wa miti na uchomaji wa misitu, hatua ambazo ni muhimu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi yanayochangia majanga kama kimbunga na ukame.
Katika hatua nyingine Mhe. Luhende amewahakikishia wananchi
ushirikiano usiokoma, upendo wa dhati na dhamira ya kweli ya kuwaletea
maendeleo kwa vitendo, huku akisisitiza kuwa ofisi yake itaendelea kuwa karibu
na wananchi katika nyakati za furaha na changamoto.




.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Post a Comment