" SHY TALENT FILMS YAENDELEA NA MAZOEZI YA KUENDELEZA VIPAJI MBALIMBALI IKIWEMO FILAMU NA TAMTHILIA SHINYANGA

SHY TALENT FILMS YAENDELEA NA MAZOEZI YA KUENDELEZA VIPAJI MBALIMBALI IKIWEMO FILAMU NA TAMTHILIA SHINYANGA

Kikundi cha sanaa cha SHY TALENT FILMS leo Ijumaa Januari 16, 2026 kimeendelea na mazoezi mbalimbali ya utayari, ikiwa ni maandalizi ya kutengeneza filamu au tamthilia mpya zitakazolenga kuelimisha jamii kupitia sanaa.

Mazoezi hayo yamefanyika katika mazingira ya nidhamu na ushirikiano mkubwa miongoni mwa wanakikundi, yakilenga kuimarisha uigizaji, mawasiliano ya jukwaani pamoja na uelewa wa ujumbe unaotarajiwa kufikishwa kwa jamii.

Mazoezi hayo yamehudhuria na Mtendaji wa Mtaa wa Miti Mirefu, Angelight Emmanuel Mwanri, ambaye baada ya kushuhudia mwenendo wa mazoezi amewapongeza vijana hao kwa juhudi na ari waliyonayo, huku akiwatia moyo kuendelea kujifunza, kufanya kazi kwa bidii na kutokukata tamaa katika safari ya sanaa.

Kwa upande wa uongozi wa kikundi, mazoezi ya leo yameshirikiwa na Katibu wa SHY TALENT FILMS Daniel Sibu, Mkurugenzi wa Misalaba Media Mapuli Misalaba, Mwenyekiti wa SHY TALENT FILMS Daniel Elimboto, pamoja na walimu wa kikundi hicho akiwemo John Jackson, ambao wameendelea kutoa miongozo na maelekezo kwa wanakikundi ili kuhakikisha kazi zinazotarajiwa zitakuwa na ubora na maudhui yenye tija kwa jamii.

SHY TALENT FILMS inaendelea kujipambanua kama jukwaa la kukuza vipaji vya vijana na kuitumia sanaa kama nyenzo ya kuelimisha, kuhamasisha na kuijenga jamii ya Manispaa ya Shinyanga na Tanzania kwa ujumla.

Mazoezi hayo yanaendelea kesho Jumamosi katika ofisi ya Misalaba Media ilizopo Mjini Shinyanga karibu na Stand ya Zamani, kuanzia saa kumi kamili jioni.

 Mtendaji wa Mtaa wa Miti Mirefu, Angelight Emmanuel Mwanri, akipongeza kwa mazoezi hayo.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post