Chemba ya Taifa ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TNCC) amezindua rasmi Sera ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabia ya nchi ya mwaka 2026, yenye lengo la kuimarisha ulinzi wa mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta ya biashara nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa sera hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Rais wa TNCC, Bw. Vicent Minja, amesema sera hiyo imelenga kuziwezesha biashara kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto za mazingira huku zikiendelea kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa.
Bw. Minja amesema kupitia sera hiyo, TNCC amelenga kujenga misingi imara ya biashara endelevu (Sustainable Business Practices) zitakazohakikisha maendeleo ya uchumi yanaenda sambamba na uhifadhi wa mazingira na ustawi wa jamii.
“Sera hii imekuwa nyenzo muhimu kwa sekta binafsi kuhakikisha shughuli za biashara zinafanyika kwa kuzingatia mazingira, kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na kuchangia maendeleo endelevu ya taifa,” amesema Minja.
Katika hafla hiyo, TNCC pia ilitambua na kuzipongeza kampuni mbalimbali zinazotekeleza biashara jumuishi na dhana ya Uchumi Rejeshi (Circular Economy), hatua inayolenga kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika mifumo ya uzalishaji na matumizi rafiki kwa mazingira.
Hatua hiyo inalenga kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi, kulinda rasilimali za mazingira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa kijani nchini.
Uzinduzi wa sera hiyo unatarajiwa kuwa chachu kwa wafanyabiashara na wawekezaji nchini kuoanisha shughuli zao na ajenda ya taifa ya maendeleo endelevu, sambamba na malengo ya kimataifa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


.jpg)
Post a Comment