" KANALI YAHYA KIDO: KAYA 15,274 ZENYE WANUFAIKA 67,718 KUWEZESHWA NA SERIKALI KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE KAGERA, KAYA 6,812 TAYARI ZIMESAJILIWA

KANALI YAHYA KIDO: KAYA 15,274 ZENYE WANUFAIKA 67,718 KUWEZESHWA NA SERIKALI KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE KAGERA, KAYA 6,812 TAYARI ZIMESAJILIWA



Na Fabius Clavery, Misalaba Media-Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Kanali  Yahya Ramadhan Kido, ametoa maagizo mazito kwa wataalam na viongozi wanaosimamia mchakato wa utambuzi wa kaya zisizo na uwezo  wa kulipia  Bima ya afya kwa wote  kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao bila vikwazo vyovyote. 


Agizo hilo linahusiana na utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, unaolenga kuhakikisha wananchi wote, hususan wasio na uwezo wa kifedha, wanapata huduma za afya bila kubebeshwa mzigo wa gharama.

‎Akizungumza mkoani katika kikao cha baraza la Ushauri cha mkoa (RCC) Februari 24 2026,Kanali Kido amesema jumla ya Kaya 15,274 Zenye wanufaika 67,718. Amesema zoezi la kuandikisha kaya hizo linaendelea na hadi Februari 20 mwaka huu Jumla ya Kaya 6,812 zenye wanufaika 18,965 zimeandikishwa.

‎Mkuu huyo wa mkoa amendeelea kusisitiza kuwa mchakato wa kutambua kaya nyingine zinazostahili kusamehewa kulipia bima ya afya unapaswa kufanyika kwa uadilifu, uwazi na haraka.

‎Mkuu huyo wa mkoa amewataka viongozi wa wilaya, watendaji wa kata pamoja na wataalam wa ustawi wa jamii kushirikiana kikamilifu katika kuoa zaidi elimu kwa wananchi juu ya Umuhimu kwa Bima Ya Afya kwa Wote.

‎Misalaba Media Imezungumza na Baadhi ya Wananchi mjini Bukoba mkoani kagera  kuhusu Bima ya afya  ambao wameiomba serikali kuhakikisha inaratibu masula muhimu Ikiwemo Dawa hosipitalini ili wananchi waepuka maswala ya kuelekezwa Kununua Dawa nje ya Hospitali pamoja na Vituo vya Afya.

‎Kwa sasa, mchakato wa utambuzi unaendelea katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo, huku mamlaka zikitoa wito kwa wananchi kushirikiana na kutoa taarifa sahihi ili zoezi hilo lifanyike kwa haki na kwa wakati.

‎Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote ni mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wote, Wanufaika sita watalazimika kulipa kiasi cha Shilingi 150,000 kwa mwaka mmoja. Kupitia mpango huu, kaya maskini zitagharamiwa na serikali ili ziweze kujiunga na mfumo wa bima ya afya na kupata matibabu katika vituo vilivyosajiliwa bila kulazimika kulipa papo kwa papo.





Post a Comment

Previous Post Next Post