" KIKAO CHA 6 SERIKALI MTANDAO CHAJIWEKEA MIKAKATI LUKUKI

KIKAO CHA 6 SERIKALI MTANDAO CHAJIWEKEA MIKAKATI LUKUKI

Na, Egidia Vedasto,

Misalaba Media, Arusha.

Katibu mkuu kiongozi  Dkt.Moses Kusiluka amesema licha ya mafanikio makubwa yaliyopo kwa sasa katika serikali mtanadao eGA bado ushirikiano wa kina unahitajika  baina ya taasisi za elimu ya juu na taasisi za serikali  ili kuweza  kuendeleleza tafiti mbalimbali zinazobuniwa ili zilete tija ndani ya nchi na kuingiza kipato badala ya kutoa huduma tu.


Pia amesema Ushirikiano huo utawezesha  kuzalisha wataalamu wabobezi watakaoendeleza mifumo hiyo na kuiweka nchi  katika rekodi nzuri ya dunia.

Akizungumza katika kikao hicho kilichokutanisha wadau wa serikali mtandao wapatao 1400 Jijini Arusha amesema serikali ya awamu ya sita chini Dkt. Samia Suluhu Hassan, sekta ya TEHAMA imepewa kipaumbele na kufanikiwa kuwa katika nafasi nzuri ya nchi zinazofanya vizuri katika matumizi hayo.Amesema lengo la mafanikio yaliyofikiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa urahisi na haraka.

"Tunajivunia kuona kwa asilimia 80 ya huduma mbalimbali serikalini zikitolewa kwa mifumo TEHAMA, hii ni ishara kubwa kwamba tumepiga hatua katika hilo na matarajio ni kusonga mbele zaidi na kuwa kinara wa nchi zilizoimarika katika matumizi ya teknolojia" amesema.


Vilevile Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya mamlaka ya serikali mtandao Dkt.Mussa Kisaka amesema kuwa ili kufikia mafanikio yanayotarajiwa ushirikiano na mashikamano ni muhimu zaidi.

Amesema katika kikao hicho majadiliano ya uwajibiakaji yatafanyika, na kuweka maazimio yatakayoboresha mamlaka  hiyo.

"Ninaahidi kuwa mshirika wenu kila mara mtakaponihitaji" amesema Dkt. Kisaka.

Katika namna hiyohiyo Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya serikali mtandao nchini Eng. Benedict Ndomba amesema mamlaka hiyo iytaendelea kuwajibika kwa kuzingatia haki, sheria na taratibu kama zilivyowekwa.


Hata hivyo ameeleza kuwa maendeleo ya matumizi ya tehama yameipunguzia seriakali mzigo wa gharama za uendeshaji majukumu yake.

"Hii ni mara ya pili Tanzania kutambuliwa na Benki ya dunia kwa ukomavu wa tehama, na sasa dunia inatutazama kwa kasi tuliyonayo,nina hakika hata kikao hiki kitaweka maazimio ya kufikia hatua kubwa zaidi"amesena Eng.Ndomba.

 

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post