Na, Egidia Vedasto,
Misalaba Media, Arusha.
Waziri wa habari, sanaa utamaduni na michezo na Mbunge was Arusha Mjini Paul Makonda amewaonya watendaji jijini Arusha kuepuka migogoro inayorudisha maendeleo nyuma kwa kiasi kikubwa.
Amezungumza hayo katika ziara yake aliyoifanya jijini humo na kukagua ujenzi wa stendi kuu ya mabasi unaotekelezwa eneo la Bondeni city Kata ya Olasiti, mradi wa barabara ndani ya Kata ya Unga Limited mradi wa ujenzi soko la Kilombero na ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri ya Jiji la Arusha.
Aidha amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo kuwa wazalendo na waaminifu kuhakikisha wanatekeleza miradi hiyo kwa wakati.
"Kila mmoja anaona kwamba Rais wetu Dkt.Samoa Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa, miradi yote hii inayoendelea kujengwa ikiwemo na soko la Morombo ni ya siku nyingi. Lakini katika hiki kifupi cha uongozi wake miradi mingi inaendelea kutekelezwa ya mabilioni ya pesa, wito wangu kwenu wananchi jiandaeni na changamkieni fulsa za maendeleo ili mkuze uchumi wenu na taifa kwa ujumla",
" Baraza la madiwani, Meya na Naibu meya imarisheni ushirikiano wenu, wasikilizeni wananchi na kuwafungulia milango ya fulsa, sitapenda kusikisikia mkirumbana katika jambo lolote, kwa maana migogoro inarudisha nyuma maendeleo"amesema Waziri Makonda.
Hata amekamilisha ziara yake kwa kuwataka Wakandarasi wanaojenga miradi hiyo kufanya kazi kwa haraka na kwa ufanisi hata kama pesa zitachelewa. Wakandarasi hao ni wazawa wanaoaminiwa na wameshatekeleza miradi mingi nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Arusha ameshukuru kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo Mkoani humo na kuwasihi wananchi kutumia miradi hiyo kuinua uchumi wao.
"Ni dhahiri kuwa maendeleo katika jiji letu yanaonekana, miradi inayojengwa ni mikubwa na kila aliye tayari kufanya kazi atapata pesa. Shukrani zangu za dhati ni kwake Dkt.Samia Suluhu Hassan.Tudumisheni amani na utulivu mambo mazuri yanakuja" amesema CPA.Makalla.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment