Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa wito kwa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kuhakikisha inakuwa kitovu cha ubora wa kitaaluma, utafiti na ubunifu unaolenga kutatua changamoto halisi za dunia ya leo.
Wito huo umetolewa wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bweni la wanafunzi katika taasisi hiyo.
Waziri Mkuu amesema ujenzi wa bweni hilo ni kielelezo cha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuimarisha miundombinu ya elimu ya juu pamoja na kukuza maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini. Alisisitiza kuwa miundombinu bora ya elimu ni msingi muhimu wa kuboresha mazingira ya kujifunzia, hasa katika kipindi ambacho idadi ya wanafunzi inaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka.
"Nitoa wito kwa mkandarasi na uongozi wa taasisi kuhakikisha kunakuwa na usimamizi madhubuti wa rasilimali na utekelezaji wa mradi kwa ufanisi na kwa wakati, ili bweni hilo likamilike mapema na kuanza kutumika kwa manufaa ya wanafunzi."amesema Dkt.Nchemba
Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema Taasisi ya Nelson Mandela inaendana kikamilifu na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwekeza katika sayansi na teknolojia. Ameeleza kuwa tayari Serikali imeanzisha shule za wasichana za sayansi katika mikoa yote 26 ya Tanzania, hatua inayolenga kuongeza idadi ya wanafunzi wa sayansi watakaokuja kujiunga na taasisi hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Taasisi ya Nelson Mandela Balozi Maimuna Tarishi, amesema bweni hilo linajengwa kwa kuzingatia viwango vya ubora ili kuhakikisha wanafunzi wanapata makazi salama na yanayowezesha kujifunza, kufanya utafiti na ubunifu kwa utulivu.
Balozi Tarishi ameongeza kuwa bweni hilo litakuwa na vyumba 184, ambapo vyumba 160 vitakuwa vya kujitegemea (self-contained), na vyumba 20 vitakuwa maalumu kwa wanafunzi wenye watoto wadogo na wenye mahitaji maalumu (apartment).

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment