" TAKUKURU KATAVI YAOKOA KIASI CHA SHS. 29,994,982/=

TAKUKURU KATAVI YAOKOA KIASI CHA SHS. 29,994,982/=





TAKUKURU Mkoa wa Katavi katika robo ya pili *Oktoba–Desemba 2025* ilifanikiwa kuokoa jumla ya kiasi cha Shs 29,994,982 kupitia shughuli za uzuiaji rushwa, uchunguzi na mashitaka.

Kati ya fedha hizo, Shs 12,000,000 zilirejeshwa baada ya kubainika kuwa mikopo ya asilimia 10 iliyotolewa na Halmashauri ya Mpimbwe kwa kikundi cha wanawake ilitumika kinyume na malengo. Baada ya ufuatiliaji wa TAKUKURU, fedha zilirejeshwa na kuwekwa katika akaunti ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu tarehe 25/11/2025.

Shs 17,994,982.19 zilirejeshwa kufuatia hatua za uchunguzi na mashitaka, ambapo washtakiwa waliingia makubaliano ya kisheria (plea bargaining). Fedha hizi zilihusisha mapato ya ndani yaliyokusanywa kupitia mfumo wa POS na zilirejeshwa katika akaunti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kwa ajili ya miradi ya maendeleo na huduma kwa wananchi.

*TAKUKURU Katavi, Februari 25, 2026*

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post