Wakati kelele na upotoshaji wa "watu wa hovyo" mitaandaoni ukijaribu kufifisha juhudi za maendeleo, Tanzania inazidi kupiga hatua za kihistoria kwa kujiimarisha kwa kutumia rasilimali zake. Ushahidi wa wazi wa ukomavu huu ni uzinduzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa Kikombo, mradi uliotekelezwa kwa fedha na wataalamu wa ndani.
Akizindua makao hayo wilayani Chamwino mkoani Dodoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa msimamo thabiti: "Hakuna uchumi imara bila ulinzi madhubuti".
Rais amebainisha kuwa uwekezaji katika miundombinu ya ulinzi ni msingi wa kulinda heshima ya Taifa, amani, na mafanikio ya kiuchumi yanayopatikana.
Licha ya changamoto za kimazingira na kijamii, Serikali ya Awamu ya Sita imeonyesha kuwa ina uwezo wa kupanga, kuamua, na kutekeleza miradi mikubwa bila kutegemea msaada wa nje.Makao Makuu ya Kikombo ni alama ya uwezo wa Tanzania kutumia rasilimali na wataalamu wake wa ndani kujenga taasisi madhubuti za kitaifa.
Katika hotuba yake ya uzinduzi Rais amesisitiza kuwa ulinzi wa kisasa hautegemei silaha pekee, bali unahitaji taarifa, teknolojia, na mifumo imara ya mawasiliano ili kukabiliana na changamoto za sasa.
Amiri Jeshi Mkuu amewahimiza Maafisa na Askari kuimarisha mshikamano na uadilifu, akionya dhidi ya mienendo inayoweza kudhoofisha imani ya wananchi kwa vyombo vyao vya ulinzi.
Rais Dkt. Samia amewataka Watanzania wote kuendelea kulinda amani na utulivu, akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya dola ndio ngao ya kweli ya rasilimali na uwekezaji unaofanyika nchini.
Uzinduzi huu ni ishara tosha kuwa Tanzania inasonga mbele kwa kasi ya mageuzi ya kiuchumi na kijamii, ikijenga misingi imara ambayo haiwezi kutikiswa na maneno ya kejeli na vitisho ya mitandaoni.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment