
Na, Seif Mangwangi Arusha
Waziri mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba amewataka wakandarasi wanaojenga miradi mbalimbali nchini kulipa stahiki za wafanyakazi wao kama walivyokubaliana kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo linalojengwa soko la kisasa la kilombero baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa stendi na soko la Kilombero, Waziri Mkuu Dkt Nchemba amesema wakandarasi wengii wamekuwa kero kwa wafanyakazi nchini.
DKT. Nchemba pia ameagiza wakandarasi wanaolipwa nyongeza ya madai yao baada ya kucheleweshewa malipo na wao wawalipe wafanyakazi wao nyongeza ya fedha Kwa muda waliokaa kusubiri malipo yao.
“ Kumekuwa na kero ya wafanyakazi kwenye miradi ya ujenzi kucheleweshewa malipo yao na pengine wameshalipwa pesa zote ila wao wakicheleweshewa fedha wanadai na fidia ya kucheleweshewa, Sasa naagiza mkishalipwa pesa zenu na wafanyakazi wenu pia muwalipe nyongeza Kwa kuwasubiria,” amesema.
Akizungumza na wananchi wa Jiji la Arusha, Dkt.Nchemba amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa Jijini Arusha.
Akiwa katika ziara yake unapotekelezwa mradi wa ujenzi wa stendi kuu ya mabasi eneo la Bondeni city iliyopo kata ya Olasiti ameelekeza ujenzi wa barabara njia nne na kuelekeza kuanza matumizi ya magari ya mwendokaai yanayotumia gesi na umeme ili kusapoti matumizi ya nishati safi.
"Miradi inayotekelezwa katika nchi italeta heshima kwa taifa letu na inadhihirisha ile kauli ya kazi na utu, kwa sasa kila mmoja anaona mageuzi makubwa katika sekta ya afya hospitali za wilaya zimejengwa 119 na kufungwa vifaa vyote, vituo vya afya 649, zahanati zaidi ya 2700, vifaa vya kibingwa katika hospitali zote za mikoa na rufaa, si hivyo tu bali hata umeme imebaki historia nzuri kwamba umeme haukatiki tena na mengine mengi ikiwemo sekta ya elimu ambayo imekuwa na mageuzi makubwa".
Kuhusu soko la Kilombero, Dkt Nchemba ameagiza wafanyabiashara waliokuwa wakitumia eneo Hilo ndio wapewe kipaumbele na kwamba ni marufuku Kwa mfanyakazi wa Serikali kukodishiwa visimba katika soko Hilo.
Kwa upande wake Waziri wa habari michezo sanaa na utamaduni Paul Makonda amempongeza Waziri mkuu kwa kuendelea kusikiliza kero za wananchi nchini na kuzipatia ufumbuzi.
Waziri Makonda amesema jiji la Arusha lina miradi 52 inayotekelezwa na inazingatia ilani ya chama cha mapinduzi (CCM).
"Waziri mkuu ndio msimamizi wa TAMISEMI hivyo kila kinachotamkwa kitatendeka ikiwemo kukamilisha barabara za ndani zenye urefu wa kilometa 13 zinazojengwa
kwa kiwango cha lami ili kurahisisha mawasiliano kuelekea mashindano AFCON.
Mkuu wa mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla amepongeza juhudi za wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maendeleo katka mkoa wa arusha.
Ameahidi kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kama ilivyoelekezwa na kuonya juu ya migogoro isiyo ya lazima baina ya wafanya biashara na baadhi ya watumishi wasio waadilifu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment