" CAG: Deni la Serikali lafikia Trilioni 110.05, Lakini Bado Salama

CAG: Deni la Serikali lafikia Trilioni 110.05, Lakini Bado Salama

 

CAG: Deni la Serikali lafikia Trilioni 110.05, Lakini Bado Salama
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere, leo Machi 30, 2026 amewasilisha Ripoti Kuu ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, katika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika ripoti hiyo, Dkt. Kichere amesema deni la Serikali limeongezeka na kufikia shilingi trilioni 110.05 kutoka trilioni 97.35 mwaka uliopita. Ameeleza kuwa ongezeko hilo limetokana zaidi na kuongezeka kwa mikopo ya nje pamoja na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani, hali iliyochangia takribani ongezeko la shilingi trilioni 2.

 

Hata hivyo, ameongeza kuwa tathmini ya uhimilivu wa deni imeonesha kuwa bado deni la Serikali lipo ndani ya viwango salama vinavyokubalika kimataifa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, thamani ya sasa ya deni la umma kwa pato la taifa ni asilimia 40.7, ikiwa chini ya ukomo wa asilimia 55, huku deni la nje kwa pato la taifa likiwa asilimia 24.9, pia chini ya ukomo wa asilimia 40.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post