
Kuimarika kwa imani ya mashirika ya kimataifa kwa utendaji wa Serikali ya Awamu ya Sita kumeendelea kuzaa matunda baada ya Benki ya Maendeleo TIB na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kusaini Hati ya Makubaliano (MoU) Machi 17, 2026 iliu kufungua fursa mpya za uwekezaji.
Hatua hii ni kielelezo tosha cha namna taasisi za kimataifa zinavyovutiwa na mazingira tulivu ya uwekezaji na juhudi za dhati za Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuukabili umaskini na kuchochea mageuzi ya kijamii na kiuchumi nchini.
Fursa mpya za uwekezaji zinaztorarajiwa kufunguliwa ni katika sekta muhimu ambazo ni mhimili wa kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja, ikiwemo nishati jadidifu, biashara ndogo na za kati (SMEs), uchumi wa buluu, pamoja na miradi ya vijana.
Kupitia mifumo bunifu ya ufadhili mseto (blended finance), ubia huu utawezesha utambuzi wa miradi yenye tija na kuongeza utayari wa uwekezaji, jambo ambalo litaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi jumuishi na kupanua fursa za ajira kwa vijana na wanawake nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Deogratius Kwiyukwa, amebainisha kuwa ubia huo unaakisi dhamira ya pamoja ya kuharakisha maendeleo endelevu kwa kutoa mitaji ya muda mrefu na suluhisho bunifu za kifedha kwa sekta muhimu za uchumi.
Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Shigeki Komatsubara, amesisitiza kuwa ushirikiano na taasisi za ndani kama TIB ni nguzo muhimu katika kuongeza athari za maendeleo, kuimarisha ustahimilivu wa kiuchumi, na kuhakikisha kuwa rasilimali zinazoelekezwa nchini zinawanufaisha walengwa kulingana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment