Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndugu
Jimotoli Jilala Maduka, ameungana na wanawake wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa
Katavi katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kwa shangwe
na matukio mbalimbali ya kijamii.
Katika maadhimisho hayo, wanawake wa Manispaa ya Mpanda
walifanya maandamano yaliyopita katika baadhi ya barabara za manispaa hiyo
kabla ya kukusanyika katika viwanja vya Ukumbi wa Manispaa ambako kulifanyika
kongamano pamoja na michezo mbalimbali ya burudani.
Miongoni mwa michezo iliyochezwa ni pamoja na kuvuta kamba,
kukimbiza kuku, kula mayai kwa kutumia kijiko, kunywa soda kwa dakika moja
pamoja na michezo mingine iliyolenga kuimarisha mshikamano, furaha na
ushirikiano miongoni mwa wanawake.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Ndugu Jimotoli Jilala
Maduka amewapongeza wanawake kwa juhudi zao katika kujiletea maendeleo pamoja
na mchango wao mkubwa katika familia na jamii kwa ujumla. Amesema wanawake ni
nguzo muhimu ya maendeleo hivyo ni muhimu kuendelea kuwapa nafasi na
kuwawezesha ili waweze kufikia malengo yao ya kiuchumi na kijamii.
Mgeni rasmi katika tukio hilo, akimwakilisha Mkuu wa Wilaya
ya Mpanda, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Fidesiana Mwanakulya amesema serikali
inaendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kuwawezesha wanawake kiuchumi ikiwemo
kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu kupitia halmashauri.
Amesema kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa
na halmashauri kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, wanawake wengi
tayari wamenufaika na kuweza kuanzisha na kuendeleza shughuli mbalimbali za
kiuchumi zinazowasaidia kuboresha maisha yao na ya familia zao.
Maadhimisho hayo yamekuwa fursa muhimu kwa wanawake kukutana, kubadilishana uzoefu na kuhamasishana kuhusu umuhimu wa umoja, mshikamano na kufanya kazi kwa bidii ili kuendelea kuleta maendeleo katika jamii.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment