Na Fabius Clavery Misalaba Media-Kagera.
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, ameagiza Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kuhakikisha wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara zao katika soko kuu la zamani wanapewa kipaumbele mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa soko jipya.
Kihongosi ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Kagera,alipotembelea mradi wa ujenzi wa soko hilo kwa lengo la kujionea maendeleo yake, akisisitiza umuhimu wa kuwatambua na kuwathamini wafanyabiashara waliokubali kupisha mradi huo.
“Naielekeza Manispaa ya Bukoba kuhakikisha wafanyabiashara waliokuwa katika soko la zamani wanapewa kipaumbele bila upendeleo wala unafiki, huku mkizingatia haki na upendo sio soko linakamilika hapa kuna kuea na watumishi ndio wamechukua vyumba nane ,” amesema Kihongosi.
Aidha, amempongeza mkandarasi anayetekeleza mradi huo kwa kazi nzuri na kasi ya ujenzi, akimtaka kuhakikisha anakamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa ili kuruhusu shughuli za kiuchumi kuendelea bila usumbufu.
Awali, akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi huo, msimamizi wa ujenzi, Nixon Kissa, amesema kuwa soko hilo linagharimu shilingi bilioni 18.9 na lilianza kutekelezwa Oktoba 2025, likitarajiwa kukamilika Januari 2027.
Ameeleza kuwa hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 19.4 na unatekelezwa na kampuni ya Dimetoclasa Real Hope Limited kwa muda wa miezi 15.
Kissa ameongeza kuwa soko hilo litakapokamilika litakuwa na vizimba 1,848 vya biashara, maduka 234, mabucha 12 pamoja na huduma mbalimbali za kijamii zitakazoboresha mazingira ya biashara kwa wakazi wa Bukoba.
Kwa upande wao, baadhi ya wakazi wa Bukoba wamepongeza mradi huo wakisema utasaidia kukuza uchumi wao. Mmoja wa wakazi hao, Juster Joseph, amesema soko la zamani lilikuwa chakavu na halikidhi mahitaji ya wafanyabiashara.
Ujenzi wa soko kuu la Bukoba ni miongoni mwa miradi minne inayotekelezwa katika Manispaa ya Bukoba chini ya Mradi wa Kuboresha Miundombinu ya Ushindani wa Miji Tanzania (TACTIC). Miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 10, kituo cha mabasi Kyakailabwa, pamoja na kingo za mto Kanoni.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
.jpg)



Post a Comment