Kesho tarehe 1/04, anga la Mbinga mji litawaka moto wa soka wakati pazia la mashindano ya Wailes Super Cup litakapofunguliwa rasmi. Kabla hata mpira haujagusa nyasi, tayari mvutano umeanza nje ya uwanja kupitia sauti za wasemaji wa timu mbili zinazotarajiwa kukutana—Mbinga Combine na Majimaji Heroes. Kisugu, shabiki kindakindaki wa Simba SC, ameapa kuiongoza Mbinga Combine kwa morali na maneno makali, huku akijinasibu kuwa uzoefu na mapenzi yake ya soka vitawapa ushindi wa kishindo.
Upande wa pili, Keivoo, shabiki sugu wa Yanga SC, ameibuka kifua mbele kuitetea Majimaji Heroes. Akiwa na jazba na kujiamini kupita kiasi, Keivoo amesema timu yake haitakuja kushiriki bali kushinda, akisisitiza kuwa Mbinga Combine hawana uwezo wa kuhimili presha ya mechi ya ufunguzi. Kauli zake zimezua gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki, zikichochea hisia kali na kuongeza hamasa kuelekea pambano hilo linalosubiriwa kwa shauku kubwa.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment