" MALIMA AITAKA COPRA NA WAKULIMA KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO YA VIUNGO KWA TIJA

MALIMA AITAKA COPRA NA WAKULIMA KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO YA VIUNGO KWA TIJA

Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaMkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Kighoma Malima, ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) pamoja na wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao ya viungo kwa kuzingatia ubora, tija na ushindani wa soko la kimataifa, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kufikia dira ya Taifa ya kukuza uchumi kupitia sekta ya kilimo.Akizungumza katika mkutano wa wadau wa mazao ya viungo uliofanyika mkoani Morogoro, Malima amesema ni lazima wakulima washirikishwe kikamilifu katika kupanga na kutekeleza mikakati ya kilimo, huku akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mifumo rafiki ya kifedha itakayowawezesha kumudu gharama za uzalishaji hasa kwa mazao yanayochukua muda mrefu kukomaa kama pilipili manga.Amesema ili kuongeza ushindani wa mazao ya viungo katika soko la dunia, kuna haja ya kuimarisha vyama vya ushirika, kuboresha mbinu za kilimo na kuhakikisha wakulima wanapata elimu sahihi ya kilimo cha kibiashara pamoja na upatikanaji wa masoko ya uhakika.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa COPRA, Irene Mlola, amesema mamlaka hiyo imejipanga kuongeza uzalishaji wa mazao ya viungo kutoka tani 22,000 za sasa hadi kufikia tani 50,000 ifikapo mwaka 2030, sambamba na kuongeza ubora na thamani ya mazao hayo kupitia uchakataji.Mlola amesema kwa sasa thamani ya mauzo ya nje ya mazao ya viungo imefikia takribani shilingi bilioni 497, huku akibainisha kuwa bado kuna fursa kubwa ya kupanua uzalishaji ili kunufaika zaidi na soko la dunia linalokadiriwa kufikia tani milioni 11 ambapo Tanzania inauza tani 1.Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Batilda Burian, amesema ni wakati wa Tanzania kuacha kuuza mazao ghafi na badala yake kuongeza thamani kupitia uchakataji, akieleza kuwa mazao ya viungo yana fursa kubwa katika sekta za afya, lishe na vipodozi.Amesema ukuaji wa soko la bidhaa za asili duniani, ikiwemo superfoods, unatoa nafasi kwa nchi kuongeza uzalishaji na kuimarisha ushindani, huku akihimiza uwekezaji zaidi katika teknolojia ya uchakataji ili kuongeza mapato na ajira.Kwa upande wao, baadhi ya wakulima walioshiriki mkutano huo wamesema licha ya uwepo wa fursa nyingi katika kilimo cha mazao ya viungo, bado wanakabiliwa na changamoto za miundombinu duni ya barabara, ukosefu wa maghala ya kuhifadhi mazao pamoja na bei zisizo na ushindani kutokana na uwepo wa madalali wachache sokoni.Wamesema kuna haja ya kuimarishwa kwa mafunzo ya kilimo cha kisasa, upatikanaji wa pembejeo bora na mifumo madhubuti ya masoko ili kuwawezesha kuongeza uzalishaji na kunufaika zaidi na sekta hiyo yenye mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa.COPRA imewakutanisha wadau ili kuweka juhudi za pamoja kuimarisha kilimo cha mazao ya viungo na kuongeza uzalishaji wenye tija unaolenga kufaidika na soko la ndani na lile la Kimataifa.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post