" Rais Dkt. Samia amemwaga fursa nyingi kwa vijana - Mkalipa

Rais Dkt. Samia amemwaga fursa nyingi kwa vijana - Mkalipa

Na: Mwandishi Wetu, PanganiFursa nyingi za uwezeshaji vijana kiuchumi zimemwagwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika maeneo mbalimbali nchini ili vijana waweze kuwa na vipato vya uhakika. Hayo yamesemwa na Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilaya ya Pangani, Nasri Mkalipa katika ziara ya kiutendaji aliyoifanya Machi 29, 2026, katika Kata za Bweni na Ubangaa wilayani Pangani.Mkalipa amesema ni dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwafanya vijana kuwa na uchumi imara ndiyo maana ameboresha sekta za elimu, utoaji mikopo ya elimu, fursa za ajira ili vijana wawe na maisha mazuri. "Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais wa aina yake. Ameongeza fursa nyingi za uwezeshaji uchumi kwa vijana na wanawake ili wawe na uchumi imara. Miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa inawagusa vijana, hivyo ni jukumu letu vijana kutumia fursa hizo kuboresha maisha yetu," amesema Mkalipa.Sambamba na hilo, Mkalipa amewaasa Vijana kujiepusha na makundi hatarishi bali wajiunge katika vikundi ili serikali iwawezeshe kwa urahisi. "Anzisheni vikundi vyenu na andiko la mradi ili serikali iweze kuwawezesha mikopo ambayo serikali inaitoa ya asilimia kumi kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu," amesema.Sanjari na hilo, Mkalipa amewakumbusha vijana kuwa mstari wa mbele kuijenga taasisi yao ya CCM ili iwe imara zaidi katika kuwatumikia wananchi. Vijana kwa upande wao wameipoingeza ziara hiyo ya Katibu wa Vijana kwani imewafanya kuwa na uelewa wa masuala mengi ya Chama na mipango inayofanywa na serikali katika kuboresha maendeleo ya nchi yetu. Katibu huyo wa Vijana ameingia siku ya sita kati ya siku tisa alizonazo za kufanya ziara ya kiutendaji katika wilaya nzima ya Pangani.


 

Post a Comment

Previous Post Next Post