" AFRIKA: TIMU 10 ZAFUZU FIFA WORLD CUP 2026

AFRIKA: TIMU 10 ZAFUZU FIFA WORLD CUP 2026





Kwa mara ya kwanza katika historia, Bara la Afrika litakuwa na uwakilishi idadi ya Timu nyingi katika fainali za FIFA World Cup 2026, baada ya timu 10 kufuzu kufuatia upanuzi wa mashindano hayo.

Timu tisa zilipata tiketi za moja kwa moja kupitia michuano ya kufuzu ya Confederation of African Football, ambazo ni Algeria, Cape Verde, Ivory Coast, Misri, Ghana, Morocco, Senegal, Afrika Kusini na Tunisia.

Nafasi ya kumi imechukuliwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo), ambayo imeandika historia kwa kufuzu baada ya kuifunga Jamaica bao 1-0 katika hatua ya intercontinental playoff. Bao hilo la ushindi lilifungwa katika muda wa nyongeza na kuipeleka DR Congo kwenye Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974

Kwa ushindi huo, DR Congo imekuwa moja ya timu za mwisho kukata tiketi yake, ikiungana na mataifa mengine ya Afrika katika mashindano hayo yatakayofanyika Marekani, Canada na Mexico.

Hatua hiyo inaifanya Afrika kuweka rekodi mpya ya kuwa na timu nyingi zaidi kuwahi kushiriki Kombe la Dunia.

Post a Comment

Previous Post Next Post