Msanii wa muziki Anjella amefunguka mengi kuhusu mabadiliko ya safari yake ya muziki, akieleza kuwa ameamua rasmi kuachana na muziki wa Bongo Fleva na kuanza kujikita katika muziki wa Injili. Akizungumza kwa njia ya simu na Misalaba Media, Anjella amesema uamuzi huo umetokana na wito wa ndani pamoja na mabadiliko ya kiimani yaliyomfanya aone ni wakati sahihi wa kubadili mwelekeo wa kazi yake ya sanaa.
Aidha, Anjella ameeleza kuwa licha ya kupokea ofa mbalimbali za kusainiwa na lebo tofauti za muziki, ameamua kuzikataa ili aweze kusimamia kazi zake kwa uhuru zaidi. Amesisitiza kuwa kwa sasa anahitaji nafasi ya kufanya muziki anaouamini bila masharti, huku akiahidi mashabiki wake kuendelea kuwapa kazi bora zenye maudhui ya kujenga na kuelimisha jamii.

Post a Comment