" ASKOFU SHOO: RIPOTI YA UCHAGUZI 2025 NI HATUA MUHIMU YA MARIDHIANO NA AMANI TAIFA

ASKOFU SHOO: RIPOTI YA UCHAGUZI 2025 NI HATUA MUHIMU YA MARIDHIANO NA AMANI TAIFA

 

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Shoo, amesema ameipokea kwa furaha ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akieleza kuwa imekuwa hatua muhimu katika kuliponya Taifa kutokana na majeraha yaliyojitokeza kipindi hicho.

Amesema ripoti hiyo imeweka wazi ukweli wa matukio yaliyotokea pamoja na kutoa mapendekezo yenye tija, ambayo yanaweza kusaidia kuimarisha misingi ya haki, uwazi na maridhiano nchini.

Dkt. Shoo ameongeza kuwa iwapo Serikali itachukua hatua stahiki na kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa, Tanzania itaendelea kubaki kuwa kisiwa cha amani, mshikamano na utulivu miongoni mwa wananchi wake.

Post a Comment

Previous Post Next Post