Diwani wa Kata ya Mwagi wilaya ya kwimba Mkoani Mwanza Masumbuko Shigita amewataka jeshi la Sungusungu kudumisha amani katika maeneo yao wananchi waendelee na uzalishaji bila ya bughudha ili kuchochea maendeleo.Akizungumza na jeshi hilo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jana kwa lengo la kumpata Mwenyekiti Kanda ya Nyambiti Shigita aliwataka Viongozi waliochaguliwa kuhakikisha wanaimarisha ulinzi kwa kiwango cha kutosha katika maeneo yao.Shigita alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kudumisha amani na utulivu katika taifa letu hivyo kuwezesha ushiriki wa wananchi katika shighuli za uzalishaji mali kwa nguvu.Katika uchaguzi huo Kisela lutambi alishinda kwa kura 55 dhidi ya mpinzani wake aliyepata 35 na hivyo kuhitisha ushindani uliokuwa mkubwa baina ya wagombea hao wawili.Lutambi alisema atahakikisha anasimamamia ulinzi kwa kushirikiana na Sungusungu wenzake ili kuendelea kudumisha amani kwani ni matumaini yake kuwa hali itakuwa shwari muda wote.Aliwapongeza sungusungu wenzake kwa kuona anafaa kuwaongoza kwa kipindi hiki na hivyo aliwaomba wampe usjirikiano.awatumikie vizuri.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment