" MPANDA: KAMATI NDOGO YA UFUATILIAJI YAKETI KIKAO CHA DHARULA KUJADILI MAENDELEO YA SHULE YA SEKONDARI NA UFUNDI MILALA

MPANDA: KAMATI NDOGO YA UFUATILIAJI YAKETI KIKAO CHA DHARULA KUJADILI MAENDELEO YA SHULE YA SEKONDARI NA UFUNDI MILALA


Mpanda. Kamati Ndogo ya Ufuatiliaji wa Shule ya Sekondari na Ufundi Milala imefanya kikao cha dharura tarehe Aprili 1, 2026, kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya shule hiyo, hususan upangaji na upimaji wa eneo la shule kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati.

Kikao hicho kilifunguliwa na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mpanda, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, ambaye aliwakaribisha wajumbe na kuwataka kuwa watulivu wakati wa kikao pamoja na kuchangia mada zilizowasilishwa kwa lengo la kufanikisha maamuzi yenye tija.

Katika hatua ya utambulisho, Katibu huyo aliwatambulisha wajumbe mbalimbali wa kamati ndogo ya ufuatiliaji ili kujenga uelewano na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka aliwasilisha agenda ya upangaji na upimaji wa eneo la Shule ya Sekondari na Ufundi Milala, akieleza umuhimu wa zoezi hilo katika kuweka msingi imara wa maendeleo ya shule hiyo. Wajumbe wa kamati hiyo waliunga mkono agenda hiyo na kusisitiza kuwa upangaji na upimaji wa eneo la shule ni hatua muhimu itakayowezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ufanisi.

Aidha, kikao hicho kilijadili suala la upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kugharamia zoezi la upangaji na upimaji, ambapo wajumbe walikubaliana kupambana kwa pamoja kuhakikisha fedha zinapatikana. Kamati hiyo ilitoa wito kwa wadau mbalimbali na wananchi wenye mapenzi mema na maendeleo ya elimu kujitokeza kuchangia ili kufanikisha zoezi hilo muhimu kwa mustakabali wa shule hiyo.

Mwenyekiti aliwashukuru wajumbe kwa mahudhurio yao, michango, mawazo na mapendekezo yao yaliyolenga kuboresha ufuatiliaji wa maendeleo ya Shule ya Sekondari na Ufundi Milala pamoja na kuimarisha shughuli za Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mpanda.

Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda na Mwenyekiti wa kikao hicho, akifungua kikao cha dharura.Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, akiwasomea wajumbe agenda katika kikao cha ufuatiliaji wa Shule ya Sekondari na Ufundi Milala.Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda na mjumbe wa Kamati Ndogo ya Ufuatiliaji wa Shule ya Sekondari na Ufundi Milala, akichangia agenda katika kikao hicho huku akiwahimiza wajumbe kuwa na umoja na mshikamano ili kuhakikisha mradi wa shule unapangwa na kupimwa, hatua itakayowezesha kupatikana kwa hati miliki ya shule hiyo. Aidha, alisisitiza kuwa kwa nia na ushirikiano, malengo hayo yanaweza kufikiwa.Ndg. Rashid Masoud Nsekela, Mhandisi wa Maji kutoka Bonde la Ziwa Rukwa, akitoa maelekezo katika kikao cha ufuatiliaji wa Shule ya Sekondari na Ufundi Milala kuhusu masuala ya bonde la maji, hususan namna sahihi ya upimaji wa eneo la shule.




 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post