Na: Mwandishi Wetu, PanganiHatimaye Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilaya ya Pangani mkoani Tanga, Nasri Mkalipa, amehitimisha ziara yake ya siku tisa katika Kata zote 14 za wilaya ya Pangani, ambapo fungakazi ya ziara hiyo imehitimishwa katika Kata za Pangani Mashariki na Pangani Magharibi, Machi 31, 2026, huku wanachama na wananchi wakijitokeza kumsikiliza.Katika hitimisho la ziara yake, Mkalipa ameendelea kuwasisitiza vijana na wanachama wa CCM kujivunia Chama chao kilichoaminiwa na wananchi kuwaongoza katika kipindi cha miaka mitano 2025-2030. Aidha, amesisitiza Chama kina wajibu wa kufuatilia miradi inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali. "Tembeeni kifuambele kwani wananchi wana imani na Chama chetu (CCM), tufuatilie miradi mbalimbali kwani serikali hii imetokana na CCM," amesisitiza Mkalipa.Sambamba na hilo, Mkalipa amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Pangani ambaye pia ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, kwa kuwa bega kwa bega na UVCCM. "Mbunge wetu Jumaa Aweso yupo pamoja na Jumuiya yetu ya vijana, na Aprili 4, 2026, tutazindua mashindano ya mpira wa miguu ya Aweso Vijana Cup na yeye (Jumaa Aweso) ndiye mdhamini wa mashindano hayo," amesema Mkalipa.Katika hatua nyingine, wanachama na wananchi wa Kata za Pangani Mashariki na Pangani Magharibi wameeleza kufurahishwa na ziara hiyo kwani imewajengea uwezo wa kufahamu masuala mengi ya Chama na serikali katika kuchochea maendeleo ya Jimbo la Pangani.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment